1 Januari 2012 Tamko la mwaka 2012"...Tarehe 4 Disemba 2011 Sekretariati ya chama imeanza kikao chake cha kwanza kwa mwaka 2012 chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu kupokea taarifa kuhusu hali ya siasa na mwelekeo taifa na chama katika mwaka mpya. Sekretariati ya chama imefanya maamuzi mbalimbali kuhusu masuala ya kiutendaji ya chama na kuandaa mapendekezo ya masuala mbalimbali ya kisera. ..."
21 Novemba 2011 Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya"...Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake maalum kilichofanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden, Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, kimepokea na kujadili kwa kina taarifa ya majadiliano na kupitishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011...."
14 Novemba 2011 Maoni ya Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba, 2011"... Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilichapisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 katika Gazeti la Serikali la tarehe hiyo. Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na kanuni za 80, 83 na 84 za Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2007..."
22 Mei 2011 Tamko la Waziri Kivuli, Wizara ya Nishati na Madini juu ya masuala, matukio na mwelekeo wa Serikali kuhusu umeme katika kipindi cha mwezi Mei"...Katika kipindi cha Mwezi Mei yameibuliwa masuala na wadau mbalimbali na zimetolewa kauli kadhaa na serikali kuhusu umeme.
Baadhi ya masuala na matukio hayo ni pamoja na kuanza kwa mgawo mkubwa wa umeme, kutokutekelezwa ipasavyo kwa hatua za dharura za kuongeza uzalishaji wa umeme, tuhuma za ufisadi katika sekta husika na masuala mengine kuhusu umeme yenye kuathiri uchumi wa taifa na maisha ya wananchi hususani wa kipato cha chini.
..."
20 Machi 2011 Taarifa kwa Umma kuhusu maamuzi ya Mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA"...Kamati Kuu kilifanya kikao Markham Hotel, Dar-Es-Salaam , tarehe 19 Machi 2011. Katika kikao hiki maalumu, pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilipokea taarifa ya hali ya siasa na jamii hapa nchini, ikitilia manani zaidi taarifa ya maandamano yaliyofanyika katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa mwezi Februari/Machi 2011 na matukio yaliyojiri baada ya hapo, zikiwemo kauli mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Serikali na CCM kuhusu maandamano hayo. ..."
17 Februari 2011 Maafa ya Gongo la Mboto: Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi Wawajibike!"...Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni. Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya..."
30 Januari 2011 Tamko la Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu hali ya Taifa"...Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 29-30 Januari 2011 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (Mb), pamoja na mambo mengine, imepokea, kujadili na kutolea maazimio Taarifa ya Hali ya Siasa na Taifa kwa ujumla..."
12 Januari 2011 Tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Juu ya Mauaji ya Wananchi wakati wa Maandamano ya Amani yaliyofanyika Arusha tarehe 5 Jan, 2011"...Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Jiji la Arusha. Tarehe 5 Januari 2011 ni siku ambayo haitasahaulika katika historia ya Tanzania. Ni siku ambayo Jeshi la Polisi la Tanzania – ambalo limepewa wajibu wa kisheria wa ‘kulinda amani, sheria na utulivu, kugundua na kuzuia uhalifu, kukamata na kudhibiti wahalifu na kulinda mali za wananchi – liliamua kwa makusudi kuacha kutimiza wajibu wake kisheria na kujipa wajibu mwingine wa kuwa ni Jeshi la kuvunja amani, kukiuka sheria, kuvuruga utulivu, kufanya uhalifu na kuharibu mali za wananchi...."
11 Januari 2011 Tamko la BAVICHA Taifa kuhusu vurugu na mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi Arusha"...Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) taifa lina laani vurugu na mauji yaliyofanywa na jeshi la polisi kwa maelekezo ya serikali inayoongozwa na CCM ambayo kwa sehemu kubwa wahanga wake ni vijana wa Arusha na Watanzania wengine kwa ujumla...."
6 Mei 2010 Taarifa ya Wazee kuandamana kuunga mkono madai ya wafanyakazi, kupinga maneno ya Rais Kikwete na kulaani matendo ya walioitwa wazee wa Dar es Salaam"...Kwa busara na subira za uzee tulitarajia kwamba Rais Kikwete ama wasaidizi wake wangerekebisha kauli zao na kurejea katika ustaarabu wa kukubaliana na madai ya msingi ya wafanyakazi na kukiri kuteleza katika matamshi ya tarehe 3 Mei 2010..."
|