menuA_1
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
MikakatiA_1
Mikakati ya Chama
»CHADEMA ni msingi
»Kuandaa Viongozi
»Wabunge/Madiwani
»Kutangaza Sera
»Mfumo wa uchaguzi
»Elimu ya siasa
»Makao Makuu
»Chaguzi zijazo
b.part
MengineyoA_1
Mengineyo
»Matamko ya Chama
»CHADEMA Bungeni
»Habari Mpya
»Hotuba mbalimbali
»Makala mbalimbali
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni

Mpango Mkakati wa Kwanza kwa 2006 -2010

Lengo ni Kuimarisha/Kujenga mtandao wa chama kwa kufungua matawi katika wilaya na kutoa mafunzo kwa viongozi na wanachama kwa mujibu wa "CHADEMA ni tawi":

lf.bevel rt.bevel
Mahojiano
Mkufunzi wa ‘CHADEMA ni Msingi’, David Kafulila ambaye pamoja na mambo mengine, anazungumzia sababu za kuanzishwa kwa mpango huu.
lf.bevel rt.bevel

  1. Mchakato wa kuhakiki wanachama utafanyika ambao unaweza kuhusisha kubadilisha kadi na kutoa zingine sambamba na kusitisha utaratibu wa kutoa kadi bure. Pia zinaweza kutolewa alama mbalimbali za utambulisho kwa mujibu wa viwango vya uchangiaji bila kuleta hisia za ubaguzi.

  2. Muundo wa chama unachukuliwa kama nyenzo muhimu ya kuwezesha ufanisi na uzingatie malengo ya chama na mazingira ya kisiasa na kiutawala katika jamii: Muundo utakaohamasishwa ni ule wenye kurahisisha mawasiliano katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuwezesha ushiriki/ushirikishwaji wa wanachama hasa ngazi za chini kwa kumilikisha chama kwa wanachama. Pia muundo unaoendana na ukubwa wa chama kitaasisi na wenye kupunguza gharama za uendeshaji. Huu ndio msingi wa ujumla wa mabadiliko yaliyofanyika.

  3. Katika kipindi chote cha utekelezaji mkazo utawekwa katika kuboresha mtandao wa chama kwa kufungua na kuendesha misingi kwa mujibu wa mpango wa CHADEMA ni Msingi; Hii itahusisha kuhakiki wanachama na kutoa kadi mpya, kuimarisha mawasiliano ikiwemo kufungua ofisi katika ngazi mbalimbali, kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali, kuweka utaratibu wa kuhakikisha vikao vya chama vinaendeshwa katika ngazi mbalimbali nchi nzima, Mkazo utawekwa katika kutoa mafunzo kwa viongozi na wanachama kuanzia ngazi ya chini, Pia mkakati wa kuhamasisha chama kuwa serekali mbadala katika maeneo ambayo chama hakijashinda utafanyika kama inavyodokezwa katika masuala ya sera na sheria.

  4. Uchaguzi wa ndani ya chama utafanyika kama njia ya msingi ya kuboresha uongozi wa chama katika ngazi zote utakaoendana na kukua kwa chama kwa sasa.

  5. Katika kipindi cha miaka mitano mafunzo yatapewa kipaumbele katika maeneo mbalimbali.

  6. Hii itahusisha pia kutafakari muundo mzuri wa kuuratibu mkoa kiutendaji ikiwemo kuangalia kama mfumo wa kuwa na kanda ya Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza ufanisi. Itabuniwa mifumo mbalimbali ambayo inaweza kutumiwa kuongeza hamasa ya chama katika mkoa wa Dar es salaam.

  7. Katika kipindi hiki yataundwa mabaraza ya makundi ya kijamii ndani ya chama ya wanawake, vijana na wazee. Hii itajuisha pia uwakilishi wa walemavu unazingatiwa katika muundo wa CHADEMA.


...Mkakati wa Pili  Kuandaa viongozi

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl
footA_1