Hotuba mbalimbali za Viongozi na Wanachama
4 Julai 2011 "...Mheshimiwa Spika, naomba upokee shukrani zangu za dhati kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni na mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa mwaka wa fedha, 2011/2012, kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 99 (7) toleo la mwaka 2007..."
25 Juni 2011 "...Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kwa niaba ya Kambi ya Upinzani ninayoiongoza kuwasilisha maoni yetu kuhusu Hotuba ya Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera uratibu na bunge, Uwezeshaji na Uwekezaji pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99 (7), Toleo la Mwaka 2007..."
25 Julai 2010 "...Tunakutana leo kwa sababu ya tendo la kishujaa la mtanzania mwenzetu Dr Wilbroad Slaa kukubali ombi la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tendo hili la kishujaa la kuachia jimbo la uchaguzi ambalo alikuwa ana uhakika wa kuletetea na badala yake kugombea nafasi ya urais ambayo baadhi ya watu wametafsiri kama ni ‘kuuawa ama kujiua’ kisiasa...."
7 Machi 2010 "...Waheshimiwa viongozi wa CHADEMA na wale Serikali, awali ya yote nawapa hongera sana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi uliyopita wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kupitia chama chetu, hasa kutokana na uchaguzi mzima kutawaliwa na hila na mizengwe...."
3 Septemba 2009 "...Nafurahi kuzungumza nanyi leo, ikiwa ni miaka minne (4) toka nihutubie mkutano mkuu wa chama Agosti 13 mwaka 2006. Siku hiyo pamoja na mambo mengine tulikizindua upya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mkutano huu, pamoja na ajenda ya uchaguzi wa chama; ni wasaa mzuri wa kutathimini hali ya chama, na hali ya taifa kutoka wakati huo..."
15 Agosti 2009 "...Mchakato wa ujenzi wa barabara umeanza, viongozi wa CCM wanaanza kuweweseka na kudai kuwa wanatekeleza ilani ya CCM. Mimi nawaambia viongozi wenzangu, mnapaswa kuwauliza ni wapi ndani ya Ilani ya CCM wameahidi kujenga barabara ya Mwandiga - Manyovu kwa kiwango cha lami? Hakuna! Mimi najua nimefanya nini kuhakikisha hili linafanyika! Ndio sababu mlinichagua..."
13 Machi 2008 "...Nchi yetu iliingia katika mfumo wa vyama vingi tena mwaka 1992, lakini pamoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, sheria zetu hazikubadilika vya kutosha kulingana na hali halisi hivyo kutokidhi mahitaji ya chaguzi zilizofuata na zinazoendelea kufanyika ili kutoa fursa sawa au uwanja tambarare wa kisiasa kwa vyama vyote..."
8 Machi 2008 "...Ufisadi sasa ni janga la kitaifa. Na Taifa linapoangamizwa na mafisadi mwathirika wa kwanza ni mwanamke. Leo hii serikali inashindwa kuboresha huduma za maji, Serikali inashindwa kusomesha madaktari, serikali inashindwa kutoa dawa zakutosha kwenye zahanati zetu, tunalea watoto waliothirika kwa utapia mlo, tunapoteza watoto kwa magonjwa yanayotibika kama maralia, wanawake wanahangaika vijijini kwa kilimo cha jembe la mkono..."
13 Agosti 2006 "...Waheshimiwa wananchi, tulishuhudia matumizi makubwa ya nguvu za serikali katika uchaguzi huo. Tulishuhudia matumizi makubwa ya majeshi yetu katika kuvuruga demokrasia na haki ya wananchi kuchagua. Tulishuhudia matumizi yasiyo na mipaka na fedha katika uchaguzi mkuu...."
25 Juni 2006 "...Leo ni siku yenye furaha sana kwenu, ni maadhimisho ya sikukuu ya wanawake wa kikristu wa Moravian kanda ya kusini kama sehemu ya utamaduni mliojiwekea. Lakini ni siku ya furaha pia kwangu, kwanza kwa kuwa mahali pa furaha yenu, lakini pili na muhimu zaidi kwa hadhi mliyonipa ya kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa siku hii muhimu..."
|