16 Mei 2012 Kauli ya Shibuda imetushtua"...BAVICHA imepokea kwa mshituko mkubwa kauli ya ndugu Shibuda kuwa yeye atagombea Urais na Meneja wake wa Kampeni atakuwa Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, na alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM..."
27 Aprili 2012 Jeshi la Polisi liache kulinda uhalifu "...KUFUATIA taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari Aprili 25, 2012 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Phillip Kalangi kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo linafanya uchunguzi wa kauli alizodai kuwa ni za uchochezi akidai zimetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa..."
26 Aprili 2012 Dkt. Slaa azuru kanda ya ziwa "...KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa amehitimisha ziara ya siku 10 ya kujenga chama na kukagua uhai wa chama katika mikoa mitano, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza, ambako katika maeneo mbalimbali alikopita amesimamia vikao vya kiutendaji ambavyo vimelazimika kuchukua maamuzi mazito na muhimu dhidi ya watu waliobainika kuhujumu maendeleo ya wananchi, kukihujumu chama, kuvunja katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA..."
7 Aprili 2012 Uteuzi wa wagombea wa Bunge la EALA"...Taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi wa Wajumbe watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA..."
28 Februari 2012 Ratiba ya Uteuzi Mgombea Arumeru"...Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inatoa taarifa kwa umma kuwa muda wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa wanachama wa CHADEMA wanaowania uteuzi wa chama kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki ulimalizika rasmi Februari 25, 2012..."
27 Februari 2012 Maombi ya mafunzo kwa vijana Ujerumani yanakaribishwa"...Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limekuwa na kawaida ya kutoa fursa za mafunzo ya makada wake ndani na nje ya Tanzania..."
24 Februari 2012 Kauli kuhusu mapatano ya Sugu na Ruge"...Idara ya Sanaa ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imepokea taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kuhusu mapatano baina ya Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Mb) na Rugemalira Mutahaba..."
23 Februari 2012 Serikali lazima iwajibike mauji ya Songea"...Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na kinalaani mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma tarehe 22 Februari 2011. CHADEMA kinatoa pole kwa familia za marehemu, majeruhi, walioharibiwa mali zao na wote walioathirika kwa namna au nyingine na vurugu zilizotokea..."
14 Februari 2012 Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki"...Baada ya kupokea taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juu ya kuwepo kwa uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Sekretarieti ya CHADEMA tayari imekaa na kuandaa utaratibu mzima wa uchukuaji na urudishaji wa fomu, ambao utafuatiwa na vikao vya chama, kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, kwa maana ya Kamati Kuu, katika kufanya uteuzi wa mwisho wa kumpata mgombea..."
11 Februari 2012 Kupitishwa Marekebisho Sheria ya Katiba"...Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa rai kwa umma na wanachama kuzingatia kwamba marekebisho husika ni ya hatua ya kwanza ya kuwezesha kuundwa kwa tume shirikishi ya katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa ripoti na rasimu ya katiba mpya..."
|